• Daily Service starts from 05.00AM- 7.30AM

Physical Address
Mbezi Beach- Makonde
Dar-es-salaam - Tanzania

Postal Address
P.O Box 60486
Dar es Salaam, Tanzania

Tel: +255 783 737 086

Email: info@siloamgoshen.org

Welcome to Siloam Ministry Church

MAJIRA MPYA YA KANISA

MWISHO WA UTUMWA WA MIAKA 430 WA KANISA

Kila miaka 2000 inapofika, MUNGU huwa anafuta majira iliyopo na kuanzisha nyingine ili watu na wanaadamu waache uovu wao. Katika kitabu cha (Mwanzo 7:23) tunasoma kuwa uovu uilopozidi juu ya nchi, MUNGU alifuta kila kiumbe chenye uhai na  akaanza  majira nyingine kwa kuanza kuhesabu siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza na mwaka wa kwanza, kama alivyoanza kipindi kile alipoumba mbibgu na nchi kwa siku saba (Mwanzo 1:1-31).

Katika tovuti hii utajifunza jinsi ambavyo Majira kamili ya MUNGU imerejeshwa na MUNGU kupiyia Nabii Eliya, yaani siku sahihi ya kuzaliwa YESU Kristo  ambayo ni 28 Adar,. Aidha, Utaona jisi kila mwezi wa kiungu ulivyo na siku 28 peke yake na kukomesha Uongo wa kalenda ya Julias Kaisari iliyofuatiwa na Kalenda ya Gregori na kukomesha utumwa wa kanisa wa miaka 430 (24 Februari 1582 hadi Februari 2012), utagundua pia kwamba siku za nyongeza hadi kufikia siku  tatu katika kila mwezi isipokuwa Februari ziliongezwa kwa falsafa ya kibinaadamu, kupingana na kile alichosema MUNGU. Tunamshukuri MUNGU kwa Roho ya Matengenezo, Marejesho na upatanisho (Luka 1:16-17) ambayo imerejesha Majira sahihi ya Mungu.